Idara ya Lugha na Fasihi ya Kiswahili ni mojawapo ya idara zinazojivunia ufanisi katika Shule ya Upili ya Maliki. Kuna jumla ya walimu wanane katika Idara hii akiwemo mwalimu wetu mkuu wa shule kama mwanaidara, mmoja wetu mwenye ujuzi zaidi. Idara hii ya Kiswahili ina walimu wafuatao, ambao hufanya kazi kwa umoja kutimiza malengo na azimio ya idara.
- Bi. Selina Mukenya, MWENYEKITI
- Bi. Juliet M., KATIBU
- Bw. Otieno, MWALIMU MKUU
- Bw. Wanjala
- Bw. Wanyama
- Bw. Kisiang’ani
- Bw. Welikhe
- Bi. Apiyo
AZIMIO LA IDARA
Azimio letu ni kumkuza mwanafunzi aliye na uwezo wa kujisomea, kufurahia, kuzungumza,kujivunia na kutangamana na jamii kwa kutumia lugha ya Kiswahili.ONO LA IDARA
Kuchochea ufanisi wa mwanfunzi katika lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili.MIKAKATI YA IDARA
- Umoja na Ushirikiano miongoni mwa walimu ili kukamilisha silabasi kwa wakati unaofaa
- Kukuza na kuendeleza sera ya lugha katika shule ya Maliki
- Kuhimiza utafiti miongoni mwa walimu na wanafunzi
Kwa ujumla, sisi kama wanaidara tunajivunia na kumtambua Mwalimu Mkuu kama mwanaidara ambaye pia ni mtahini wa karatasi ya tatu ya mtihani wa kitafifa wa K.C.S.E
Bi. Selina Mukenya,
Mkuu Wa Idara ya Kiswahili